MOROCCO YAKUBALI KUSHIRIKIANA NA TANZANIA KWENYE MICHEZO
Na. John Mapepele Waziri wa utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa leo Februari 15, 2022 amekutana na Balozi wa Morocco nchini Mhe. Zakaria Elgoumiri na kufanya mazungumzo ya kuendeleza sekta za michezo, utamaduni na Sanaa ambapo Balozi amesisitiza serikali yake ipo tayari kushirikiana na Tanzania kwa faida ya wananchi wa nchi hizo. Mhe. Mchengerwa amesema Serikali ya Tanzania na Morocco zimekuwa na uhusiano mzuri katika sekta hizo toka muda mrefu hali ambayo imewafanya viongozi wakuu wa nchi zote kufanya ziara na kubadilishana uzoefu wa sekta hizo. Akiwa katika kikao hicho ambacho aliambatana na Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Dkt, Hassan Abbasi, Mkurugenzi wa michezo nchini Yusufu Singo na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Michezo (BMT) Neema Msitha wamekubalina na ujumbe wa Mhe. Balozi wa kuendelea kushirikiana kwenye sekta hizo. Ameyataja baadhi ya maen...
Comments
Post a Comment