Posts

Mhe. Mchengerwa ahimiza kumuenzi Bibi Titi

Image
  Na John Mapepele Waziri Wa Utamaduni, Sanaa, Mhe. Mohamed Mchengerwa amehimiza umuhimu wa kumuenzi mwanaharakati  mwanamke, Bibi Titi Mohamed aliyefanya kazi kwa karibuni na Mwalimu Julisu Nyerere katika harakati za kuleta uhuru wa Tanganyika. Akizungumzia tamasha  la Bibi Titi Mohamed litakalofanyika  wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani, Mhe. Mchengerwa kwenye kipindi cha 360 cha kituo cha televisheni cha Clouds leo ambapo amesema  Bibi Titi ni alama ya mabadiliko katika suala zima la ushiriki wa wanakwake katika harakati hizo na kuleta mabadiliko.  “Ukimzungumzia Bibi Titi Mohamed unazungumzia alama ya mabadiliko, unazungumia alama ya kutoka kutoamini kuja katika kuamini kwa sababu Bibi Titi  mwenyewe aliamini kwamba tunaweza kujikomboa,” amesema. Amesema ni vigumu kuzungumzia mabadiliko ya kisiasa ya kuwaingiza wanawake katika siasa, ushawishi wa katika siasa, uchumi, matumizi ya Kiswahili,  bila kumzungumzia Bibi Titi Mohamed.   Amesema...

Mhe. Mhengerwa -Tamasha la Sanaa Bagamoyo ni la kimataifa, Makamu wa Rais afafanua kuwa Sanaa inaongoza katika ukuaji wa uchumi nchini

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema  Serikali imefanya  maboresho makubwa   kwenye Tamasha la mwaka huu la 41 la Utamaduni na Sanaa   Bagamoyo kuwa la kimataifa ambapo limeshirikisha nchi mbalimbali duniani ili kuitangaza Tanzania na utamaduni wake duniani. Kauli hiyo ameitoa leo wakati akimkaribisha Makamu wa Rais Mhe, Dkt. Philipo Mpango kuzindua rasmi tamasha hili kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano. Mhe. Samia  Suluhu Hassan. Ameongeza kuwa tamasha hili limeshirikisha vikundi vya wasanii kutoa mataifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Canada, Zambia, Burundi na Visiwa vya Mayote kutoka nchini Ufaransa. “Mwaka huu tumeendelea  kuliboresha Zaidi tamasha hili kutoka kuwa tamasha la mazoea la wanafunzi wa sanaa hapa chuoni ili kulipatia hadhi zaidi ya kuwa tamasha la kimataifa.” Amesisitiza Mhe. Mchengerwa Aidha amesema wameteleza maelekezo ya Mhe. Rais ya kutaka kuendeleza tamasha hili n...

Waziri Mchengerwa atoa siku 30 kwa BMT kutengeneza mifumo ya kusajili ya kielektoniki

Image
  Na John Mapepele  Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa amelielekeza Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kuhakiksha ndani ya mwezi mmoja linatengeneza mfumo wa kieletroniki wa kusajili vyama vya michezo ili kuondoa usumbufu kwa wadau unaojitokeza. Mhe. Mchengerwa ameyasema  haya  leo Oktoba 27, 2022 wakati akizindua program ya “Mpira Fursa” inayoratibiwa na Taasisi ya Karibu Tanzania (KTO) na kugawa  vifaa vya michezo kwa  Vyuo vya Wananchi vya  Maendeleo 54 kote nchini na shule za msingi 86.   Ameutaka uongozo wa shule ambazo zitabahatika kupata vifaa vya soka, kuwaruhusu wasichana kucheza soka na kuvitumia vifaa hivyo kwa uangalifu na kwa madhumuni yaliyokusudiwa.   Ameipongeza KTO kwa kuanzisha program hiyo ya kupeleka  michezo  katika vyuo vya  wananchi  vya maendeleo na shule za msingi huku akifafanua kuwa  huo ni utekelezaji wa  maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanza...

Waziri Mchengerwa azindua zoezi la kitaifa la kusaka na kuibua vipaji "mtaa Kwa mtaa."

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni,  Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa leo Oktoba 16, 2022 amezindua  zoezi la  kitaifa la  kuibua na kusaka vipaji  vya Sanaa la "Mtaa kwa Mtaa" eneo la  Ikwiriri wilayani Rufiji, zoezi ambalo litafanyika nchi nzima. Akizindua zoezi hilo katika eneo la Ikwiriri, Mhe. Mchengerwa amesema eneo linalofuata baada ya uzinduzi wa leo ni Mkoa wa Arusha ambapo litafanyika kila mtaa ili kuibua vipaji kwenye sanaa. Amewataka watanzania  wenye vipaji vya Sanaa kujitokeza wakati wa zoezi hilo likiendelea  ili waweze kuendelezwa baada ya kuibuliwa, huku akisisitiza  kauli ya Kipaji chako ndiyo mtaji wako. "Ndugu zangu hii ni ndoto ya Mheshimiwa Rais wetu, Rais anatamani kuona misingi iliyowekwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere ya kuthamini na kuendeleza Sanaa inaendelezwa ili kuwanufaisha vijana" amesisitiza,  Mhe. Mchengerwa   Amezitaka mamlaka za wilaya na mikoa kote nchini kusai...

Hafla ya kuiaga Serengeti Girls, Mhe. Mchengerwa atoa maagizo mazito kwa Mkurugenzi mpya wa Michezo

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.  Mohamed Mchengerwa leo Septemba 21, 2022 amewaongoza watanzania kuiaga timu ya Serengeti Girls  kwenda Kombe la Dunia huku akitoa maelekezo mahususi kwa Kaimu Mkurugenzi mpya wa Michezo kuhusu kuendeleza sekta hiyo. Katika hafla ya kuiaga timu hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Mhe. Mchengerwa amekabidhi BIMA na  vifaa mbalimbali  vya michezo ambapo pia Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi  na wadau mbalimbali wa michezo walishiriki. Mhe. Mchengerwa  amemtaka Kaimu Mkurugenzi mpya, Ally  Mayay kuleta maboresho kusudiwa kwenye Sekta ya Michezo na endapo hataweza ataondolewa. Mbali na hayo,  Mhe. Mchengerwa amempa  maelekezo  mahususi ambayo ametaka yafanyiwe kazi mara moja. Maelekezo hayo ni pamoja na kuweka mfumo wa Kutafuta vipaji vya wachezaji Kwa kushirikiana na Baraza la Michezo la Taifa ( BMT) na  Shirikisho la Soka nchini (TFF) pia kuandaa ...

Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo yashirikiana na Wizara ya Maliasili kuitangaza Tanzania, kukuza utalii.

Image
  Na John Mapepele Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo na Wizara ya Maliasili na Utalii leo Septemba 16 na  taasisi wadau wa Wizara hizo kutoka  pande zote za Muungano wamekutana na kufanya kikao  kujadili  namna bora ya kutumia Utamaduni, Sanaa na Michezo kukuza utalii. Kauli hiyo ameitoa Waziri wa Utamaduni,  Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa baada ya kikao hicho cha pamoja ambapo amefafanua kuwa wizara yake imekuwa na matukio makubwa ambayo yanauhusiano mkubwa  na Utalii. Aidha, amesema kuna mambo ambayo wamekubaliana  kwa mshikamano na kutekeleza kwa pamoja  kuhakikisha kuwa sekta hizo zinakua. Amesisitiza kuwa  Kwa Ushirikiano baina ya  wizara itasaidia kupeleka taifa  mbele kwa kuwa sekta hizo zinategemeana. "Sisi katika Utamaduni tunao Utamaduni wa utalii, lakini katika michezo  kuna michezo na Utalii ambapo tunapokea wachezaji mbalimbali wa Kimataifa". Ameongeza  Mhe. Waziri Amesema tayari taifa limew...

MCHENGERWA AITAKA COSOTA KUTOA ELIMU YA KANUNI MPYA ZA ADA ZA VIBEBEA KAZI ZA SANAA NA MAKAMPUNI YA WASANII

Image
  Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa ameitaka Taasisi ya Hakimiliki nchini (COSOTA)  kutoa elimu ya kutosha kwa wadau hususan wabunge      kuhusu mabadiliko makubwa yanayofanywa na taasisi hiyo ya kimuundo na kisekta ili kusaidia kuinua maisha ya wadau wa sekta ya Sanaa nchini. Waziri Mchengerwa ameyasema haya leo Septemba 14, mara baada ya kupitishwa  yeye na Naibu wake Mhe, Pauline Gekul na Menejimenti ya taasisi hiyo kwenye kikao cha kujadili  rasimu ya kanuni ya uanzishwaji wa Ada kwa vibebea kazi za ubunifu (blank device) na uanzishwaji wa makampuni binafsi ya   wasanii ya ukusanyaji na ugawaji mirahaba (CMO). Amewataka kuharakisha mchakato wa kukamilisha rasimu hizo ili  zisainiwe  na kuanza kutumika mara moja hatimaye wasani na wadau mbalimbali wa kazi za Sanaa waweze kunufaika na kazi zao. "Harakisheni, ninakwenda kuisaini kanuni hizi mara moja ili wasanii  wafaidi matunda ya...