Hafla ya kuiaga Serengeti Girls, Mhe. Mchengerwa atoa maagizo mazito kwa Mkurugenzi mpya wa Michezo
Na John Mapepele Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa leo Septemba 21, 2022 amewaongoza watanzania kuiaga timu ya Serengeti Girls kwenda Kombe la Dunia huku akitoa maelekezo mahususi kwa Kaimu Mkurugenzi mpya wa Michezo kuhusu kuendeleza sekta hiyo. Katika hafla ya kuiaga timu hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Mhe. Mchengerwa amekabidhi BIMA na vifaa mbalimbali vya michezo ambapo pia Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi na wadau mbalimbali wa michezo walishiriki. Mhe. Mchengerwa amemtaka Kaimu Mkurugenzi mpya, Ally Mayay kuleta maboresho kusudiwa kwenye Sekta ya Michezo na endapo hataweza ataondolewa. Mbali na hayo, Mhe. Mchengerwa amempa maelekezo mahususi ambayo ametaka yafanyiwe kazi mara moja. Maelekezo hayo ni pamoja na kuweka mfumo wa Kutafuta vipaji vya wachezaji Kwa kushirikiana na Baraza la Michezo la Taifa ( BMT) na Shirikisho la Soka nchini (TFF) pia kuandaa ...